Mwakinyo,Mfilipino Rekodi Zinaongea

0

Bondia Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupambana na bondia raia wa ufilipino Arney Tinampay katika pambano la uzito la Super welter litakalofanyika katika uwanja wa Uhuru nchini tarehe 29 Novemba pambano linalotarajiwa kuwa na raundi 10.

Tinampay bondia namba moja nchini humo katika uzito wa super welter hajapoteza pambano lolote la knock out(Ko) katika jumla ya mapambano 51 aliyocheza huku akipoteza mapambano 24 na akiwa na uzoefu katika kupambana na akishika nafasi ya 202 kwa ubora duniani.

Mwakinyo anayeshika nafasi 19 kwa ubora duniani atakupamba na mfilipino huyo huku akilinda asipoteze pambano hilo ili kulinda nafasi yake ya ubora duniani.

“Ni pambano gumu kwangu na nalichukulia kama pambano la kufa na kupona”Alisema Mwakinyo anayesifika kwa ngumi zito huku promota wa pambano hilo Jay msangi akiahidi kuwa na mapambano manne ya utangulizi.

Leave A Reply

Your email address will not be published.