Mchezaji wa Klabu ya Simba Sc Ladack Chasambi amefanikiwa kuteka nyoyo za mashabiki wa klabu ya Simba sc kutokana na kuonyesha kiwango bora kabisa katika mchezo baina ya klabu yake dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao Simba sc iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku Chasambi akifunga bao la tatu na kuifanya klabu hiyo kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.
Chasambi alikua na wakati mgumu katika mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate ambapo alisababisha mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1 kutokana na kujifunga bao kipindi cha pili cha mchezo huo.
Mashabiki walifurahia bao la Chasambi pamoja na kiwango alichoonyesha ambacho sasa kimemrejesha mchezoni.
Akielezea ilivyokua kabla ya mchezo huo na nini alichoambiwa na kocha Fadlu Davis wakati akimpa nafasi Chasambi alimshukuru kocha huyo kwa maelekezo na ushauri aliompa.
“Maneno yalinijenga ,nilikuwa napitia wakati mgumu Kwa tukio ambalo lilitokea Nilijisikia vizuri baada ya kufunga goli sababu nimeisaidia timu , mashabiki waendelee kutusapoti na wanisamehe Kwa kosa ambalo nilifanya”,Alisema mchezaji huyo.
“Kocha Fadlu amekuwa na mchango mkubwa sio kwangu tu ni kama mlezi Fadlu aliniambia ule mchezo umepita hatuwezi kurudisha siku nyuma ,nitakupa nafasi mchezo ujao ukafanye vizuri”,Alisema Chasambi wakati akihojiwa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Baada ya mchezo huo kumalizika mashabiki walimuita staa huyo na kumkabidhi kaput maalumu amb