Connect with us

Makala

Yanga Sc Yanukia Robo Fainali Cafcl

Ushindi wa 1-0 ulioupata klabu ya Yanga sc dhidi ya Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan umeiweka timu hiyo katika matumaini makubwa ya kufuzu robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika mchezo uliofanyika nchini Mauritania.

Yanga sc sasa inapaswa kushinda mchezo ujao dhidi ya Mc Algers utakaofanyika nchini katika uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi Januari 18 2024.

Bao pekee la mapema la kiungo mshambuliaji Stephan Aziz Ki lilidumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo huo mgumu na wenye kasi kubwa.

Uzembe wa viungo wa Al Hilal kutomkaba Azizi Ki aliyepiga shuti kali lililozama wavuni moja kwa moja dakika ya saba ya mchezo huo.

Kila upande ulikua na uwezekano wa kupata bao kutokana na timu hizo kushambuliana kwa zamu kila mara hali iliyosababisha mchezo huo kutotabirika kirahisi.

Prince Dube alikosa nafasi kadhaa za mabao baada ya kushindwa kumchungulia kipa Fofana aliyekua kikwazo kwa Yanga sc.

Yanga sc sasa imefikisha alama saba ikiwa nyuma ya Al Hilal Fc yenye alama 10 ikiwa imeshafuzu huku Mc Algers ikiwa na alama nane ikiwania kufuzu endapo itapata sare ama kudhi

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala