Klabu ya soka ya Simba Sc imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Bravos do Marquiz ya nchini Angola.
Simba sc iliruhusu bao la mapema dakika ya 13 ya mchezo kutokana na uzembe wa beki Che Fondoh Malone kushindwa kukontroo mpira eneo la hatari na mpira kumkuta mfungaji aliyeupiga kwa ustadi mkubwa ma kuwandikia wenyeji bao.

Kibu Dennis ni kama hakua na bahati baada ya kupiga vichwa viwili vilivyogonga mwamba huku pia uimara wa kipa wa Bravos ulikua kikwazo kikubwa kwa Simba sc.
Kipindi cha pili kocha Fadlu Davis alifanya mabadiliko akimtoa Ellie Mpanzu na kumuingiza Ladack Chasambi aliyeongeza nguvu ya kuzuia na kushambulia kwa kasi.
Lionel Ateba alifunga bao la kusawazisha kwa Simba sc dakika ya 69 ya mchezo na kupeleka shangwe kwa mashabiki wa Simba sc nchini.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Simba sc ilifanikiwa kuchukua alama moja na kufikisha alama 10 ambazo moja kwa moja zinawapa tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Cs Constantine.
Mchezo huo utakaofanyika Januari 19 wikiendi ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa utaamua nani awe kinara wa kundi hilo la A ambapo Simba sc akishinda basi atakua mshindi wa kwanza wa kundi hilo na endapo atapata sare ama kupoteza basi atakua mshindi wa pili wa kundi hilo.