Connect with us

Makala

Simba sc Yatakata Ugenini

Bao pekee la Jean Charles Ahoua dakika ya 34 ya mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Cs Sfaxien limeihakikishia Simba sc alama tatu katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Hammadi Agrebi nchini Tunisia.

Katika mchezo huo wa Kundi A la kombe la Shirikisho barani Afrika Simba sc ilifanikiwa kuonyesha kiwango bora na kushambulia kwa kasi kushinda wenyeji na kupata bao hilo kufuatia mpira mrefu wa Che Malone Fondoh kusetiwa vizuri na Lionel Ateba ambapo mpira ulimkuta Ahoua akiwa hajakabwa na kufunga kwa shuti kali.

Mchezo huo ulichezwa bila mashabiki kutokana na klabu hiyo kufungiwa na Caf kwa sababu za utovu wa nidhamu wa mashabiki hao.

Simba sc sasa imefikisha alama tisa ikiwa nafasi ya pili ya kundi A nyuma ya Cs Constantine wenye alama tisa lakini wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mchezo ujao ndio utaamua hatma ya Simba ambapo wataenda ugenini kuwavaa Bravos ambapo anapaswa kushinda ama kutoa sare ili kupata uhakika wa kufuzu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala