Connect with us

Makala

Mpanzu Safi Caf,Kuwavaa Watunisia

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Ellie Mpanzu amefanikiwa kupata leseni ya Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) na sasa atatumika katika mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya klabu yake na timu ya Sc Sfaxien ya nchini Tunisia.

Mchezo huo utakaochezwa kesho Jumapili mjini Tunis unatarajiwa kuwa rahisi kwa Simba sc kuchukua alama tatu ama sare kutokana na wapinzani hao kuwa na mwenendo usioridhisha kuanzia ligi kuu ya nchini mwao mpaka katika michuano ya Caf.

Mpanzu ambaye amesajiliwa na Simba sc msimu huu na kuanza kutumika wakati huu wa dirisha dogo ana uwezo wa kucheza nafasi zote za ushambuliaji kwa ufanisi zaidi.

Tangu atangazwe klabuni hapo na kuanza kucheza rasmi katika ligi kuu msimu huu Mpanzu amecheza jumla ya michezo mitatu ambapo licha ya kuongeza kasi eneo la ushambuliaji la klabu hiyo bado hajafanikiwa kufunga bao wala kutoa asisti mpaka sasa.

“Tayari tumepata ridhaa ya kumtumia Mpanzu baada ya leseni yake kutoka Caf kuwa tayari na hivyo ataanza kutumika katika michuano ya Caf kuanzia mchezo huu”.Alisema Ahmed Ally meneja habari wa klabu hiyo.

Simba sc katika kundi A la michuano ya kombe la Shirikisho mpaka sasa ina alama sita sambamba na timu za Bravos na Cs Constantine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala