Kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Sead Ramovic ameahidi kuendelea kutumia mfumo wake wa kushambulia zaidi kuelekea mchezo wa kesho wa hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Tp Mazembe utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Ramovic amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mapema siku ya leo ambapo ameonyesha kuwa klabu yake inahitaji alama tatu muhimu ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali.
“Asante sana kwa swali lako. Ndio, mtindo wangu wa uchezaji, kama wengi wanavyojua sasa ni mtindo wa kiwango cha juu wa nguvu ambapo hatutaki kuwapa wapinzani nafasi au muda, kama ulivyosema”.Alisema Ramovic
“Ni vizuri pia kuona kwamba wachezaji wanajifunza na wanaamini katika mtindo huu wa uchezaji. Wanajitahidi mazoezini, umeshacheza mechi nne za ligi vizuri. Kwa ujumla, tuko kwenye njia sahihi lakini kesho ni mechi mpya tena, yenye changamoto tofauti” . Alimalizia Sead Ramovic akijibu swali la mwandishi wa habari.

Naye mchezaji Dickson Job kwa niaba ya wachezaji wenzake alisema kuwa wao wapo tayari kuibuka na alama tatu katika mchezo huo.
“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tupo kwenye wakati mzuri kitumu, tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho na tutakwenda kupambana asilimia 100 kuhakikisha tunapata matokeo”.Alisema Job
Yanga sc inalazimika kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo kupitia kundi A ambapo Al Hilal Fc inaongoza ikiwa na alama tisa ikifuatiwa na Mc Algers yenye alama nne kisha Tp Mazembe yenye alama mbili na Yanga sc ikishika mkia ikiwa na alama moja.