Connect with us

Makala

Pamba Jiji Yarudi kwa Yondani

Beki kisiki wa zamani wa klabu za Simba sc na Yanga sc Kelvin Patrick Yondani amejiunga na klabu ya Pamba Jiji Fc yenye makao yake jijini Mwanza ili kuongeza nguvu kuelekea mechi za raundi ya pili ya ligi kuu nchini.

Kocha Fred Felix Minziro ameona kuna umuhimu wa kumsajili mkongwe huyo ambaye alikua huru kutokana na kutofikia makubaliano na baadhi ya klabu za ligi kuu baada ya timu yake ya Geita Gold Fc kushuka daraja.

Tayari mchezaji huyo ameshakamilisha dili hilo na sasa amejiunga na kambibya timu hiyo kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya michezo ya ligi kuu nchini.

Pamba Jiji Fc imeshinda mchezo mmoja pekee wa ligi kuu ikiwa na alama 11 katika nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi kuu wakiwa wamecheza michezo 13.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala