Connect with us

Makala

Dube Atupia Zimbabwe Ikishinda 3-1

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Prince Mpumelelo Dube amesaidia nchi yake ya Zimbabwe kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namibia ikiwa katika kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani nchini Algeria.

Musona ⚽⁵⁰’ ⚽⁶1′ (Penati)
Dube ⚽⁸⁹’

Eiseb ⚽⁹⁰’

Katika Mchezo huo mabao ya Zimbabwe yalifungwa na mshambuliaji Walter Musona dakika ya kwanza kwa penati huku bao la pili likifungwa na Eiseb na Dube ambaye anaichezea klabu ya yanga sc aliingia dakika 81 na 89 akifunga goli la 3.

Kuelekea kufuzu michuano hiyo,Timu ya Taifa ya Zimbabwe Inaendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lao huku wakiwa na alama 8 baada ya kucheza Michezo 4.

Baada ya mchezo huo sasa Dube anatarajiwa kuanza safari ya Kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya klabu yake kuelekea kwenye Mchezo Mkubwa wa Kariakoo derby tarehe 19 dhidi ya Simba Sc utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mbali na Dube tayari staa Stephan Aziz Ki yeye tayari ameanza safari ya kurejea nchini kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala