Connect with us

Makala

Yanga Sc Yamkana Kagoma

Klabu ya Yanga sc imekanusha taarifa za kumsamehe kiungo wa klabu ya Simba sc Yusuph Kagoma ambaye imemfungulia mashtaka katika kamati ya usajili na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kutokana na kusaini mkataba na klabu hiyo kisha kuiacha na kujiunga na klabu ya Simba sc.

Yanga sc inadai kwamba ilikubaliana na klabu yake ya Fountain Gate Fc kuhusu kumsajili mchezaji huyo na kumalizana kila kitu kisha kumsainisha mkataba mchezaji huyo ambae baadae alisaini mkataba mwingine na klabu ya Simba sc ambayo amejiunga nayo mpaka sasa huku akisema kuwa ameamua kuachana na Yanga sc sababu ya kutoiona nafasi yake kikosini humo.

Awali siku chache zilizopita uongozi wa mchezaji huyo uliishukuru uongozi wa Yanga sc kwa kukubali kulimaliza suala hilo ambapo taarifa ilisomeka kuwa “Uongozi wa Yusuph Kagoma pamoja na uongozi wa Yanga, tumefikia makubaliano ya kumaliza mgogoro wa mkataba wa usajili ambao ulikuwa ukishughulikiwa na Kamati za Hadhi za wachezaji ya TFF”

“Tunapenda kutumia nafasi hii kuushukuru Uongozi wa Klabu ya Yanga chini ya Rais wake Eng. Hersi Ally Said kwa kukubali kumsamehe mchezaji kwa maslahi mapana ya kulinda kipaji chake,Kufuatia makubaliano hayo, sasa mchezaji yuko huru kuitumikia klabu yake ya sasa Simba Sports Club, na tunamtakia kila la kheri katika safari yake mpya ya soka.”Ilisomeka taarifa hiyo.

Baada ya Taarifa hiyo kutoka,Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga sc Ally Kamwe alisema kuwa wao kama klabu hawatambua mazungumzo hayo na wanasubiria maamuzi ya kamati ya usajili na hadhi za wachezaji ya TFF.

“Hii taarifa ni ya uongo na hatujui aliyetengeneza alikuwa na dhamira gani hakuna taarifa kutoka Yanga kwamba tumemsaheme mchezaji yeyote wala makubaliano yoyote”.Alisema Kamwe huku akiendelea kuwa

“Ni kweli lipo shauri Kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji la klabu ya Yanga likimuhusu mchezaji Yusuph Kagoma na taarifa ni kwamba Kamati imekutana na kufanya maamuzi ya kumsimamisha mchezaji asiendelee kutumia Kwenye mechi za timu yake anayoitumikia.

“Kamati yenyewe inashangaa kuona mchezaji bado anatumika huku ana shauri lake chini ya kamati hiyo, nafikiri wadau na wachambuzi wa mpira wa miguu watakuwa na nafasi nzuri ya kutuelezea na kutuchambulia jambo hili”.Alimalizia kusema mkuu huyo wa Idara ya habari ya Yanga sc.

Endapo itagundulika kuwa amesaini timu mbili basi mchezaji huyo anaweza kupewa adhabu ya kufungiwa msimu mzima ama kupigwa faini huku akipaswa kurejesha fedha alizochukua katika klabu husika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala