Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Kagera Sugar Fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Yanga sc ikianza na safu ya ulinzi wa mabeki watatu wa kati huku golini akisimama Kipa Djigui Diarra na mabeki wa pembeni ambao walikua wanacheza kama mawinga walikua Chadrack Boka na Dickson Job na Khalid Aucho na Mudathir Yahaya wakiwa viungo wa kati huku Prince Dube na Pacome Zouzoua sambamba na Stephan Aziz Ki wakiongoza eneo la ushambuliaji.
Kagera Sugar walianza mchezo kwa uoga na kukaribisha mashambulizi mengi ambapo kukosa umakini kwa Prince Dube na Pacome Zouzoua kulimpa sifa kipa Ramadhan Chalamanda aliyeokoa michomo kadhaa.
Maxi Nzengeli aliiandikia Yanga sc bao la uongozi dakika ya 26 ya mchezo akimalizia pasi safi ya Pacome Zouzoua na bao hilo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili Kagera Sugar waliamka na kuja na mkakati mkali wa kumiliki mpira na kuwanyima uhuru Yanga sc ambao hawakufanikiwa kufika langoni mwa Kagera Sugar mara kwa mara.
Kocha Miguel Gamondi aliwapumzisha Dube na Pacome na kuwaingiza Clement Mzize na Cletous Chama ambaye alibadili upepo wa mchezo na kuwaamsha Yanga sc ambao walianza kushambulia kwa kushtukiza.
Yanga sc walipata bao la pili kwa juhudi binafsi za Mzize kuvumilia alipoangushwa na kumpasia Aziz Ki na kisha kuiwahi pasi ya mbele na kuihakikishia timu yake alama tatu muhimu.
Yanga sc sasa imefikisha alama tatu ikiwana mchezo mmoja huku Kagera Sugar ikiwa haina alama baada ya kufungwa michezo yote miwili ya nyumbani.