Connect with us

Makala

Yanga Sc Yairarua Vital O

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital O ya Burundi katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Yanga sc iliingia bila wasiwasi ikiwa na mtaji wa mabao 4-0 ilioupata katika mchezo wa awali hapo hapo Chamazi ambapo kocha Miguel Gamondi aliwapumzisha baadhi ya mastaa kama Khalid Aucho na Ibrahim Hamad Bacca huku Cletous Chama akiungana na Djigui Diarra,Dickson Job,Bakari Mwamnyeto,Nickson Kibabage,Aziz Andabwile,Duke Abuya sambamba na Kenedy Musonda pamoja na Clement Mzize na Pacome Zouzoua kuunda kikosi kilichoanza.

Pacome Zouzoua aliandika bao la kwanza kwa penati baada ya beki wa Vital O kuunawa mpira uliokua unakwenda wavuni na kisababisha mwamuzi kuamuru penati na kadi nyekundu kwa beki huyo dakika ya 14 ya mchezo.

Mzize alimalizia kazi nzuri ya Chama na kufunga bao la pili dakika ya 49 ya mchezo huku Chama akifunga bao la tatu kwa fault kali dakika ya 51 ya mchezo.

Prince Dube alifunga bao la nne dakika chache baada ya kuingia akimalizia pasi safi ya Chama huku Aziz Ki naye akifunga bao la tano kwa Yanga sc kwa shuti kali akimalizia tena pasi cha Chama na dakika ya 86 Mudathir Yahaya alifunga bao la sita kwa Yanga sc akimalizia tena pasi ya Chama.

Yanga sc baada ya ushindi huo imejihakikishia milioni 30 ya zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan huku pia ikifuzu hatua inayofuata kwa kishindo.

Yanga sc sasa itakutana na CBD ya nchini Ethiopia katika hatua inayofuata ambapo itaanzia ugenini na kumalizia nyumbani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala