Connect with us

Makala

Feisal Aikazia Azam Fc

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Azam Fc Feisal Salum ameigomea Klabu yake kuendelea na Mazungumzo ya mkataba mpya baada ya kuutumikia huu uliopo wa miaka mitatu kwa mwaka mmoja pekee.

Azam Fc walimnunua Feisal Salum kutoka Yanga sc kwa dau la usajili la shilingi milioni 200 ambapo ilimsainisha mkataba wa miaka mitatu huku ikiweka dau la shilingi bilioni 1.3 kwa timu ambayo itamhitaji kuunua mkataba wake klabuni hapo.

Baada ya mchezaji huyo kuutumikia mkataba wake wa miaka mitatu kwa mwaka mmoja pekee,Klabu hiyo imeona kuna haja ya kufungua Mazungumzo kwa ajili ya kuongeza zaidi mkataba huo ikihofia mchezaji huyo kuondoka pindi mkataba wake utakapomalizika.

Kiwango bora alichoonyesha staa huyo akifunga mabao 19 katika ligi kuu msimu uliopita ambapo licha ya klabu hiyo kukosa taji lolote bado binafsi kama mchezaji alifanikiwa kuonyesha kiwango bora zaidi.

Mchezaji huyo mpaka sasa amekataa Mazungumzo kuhusu mkataba mpya na klabu hiyo huku taarifa zaidi zinadai kuwa anavutiwa zaidi na mpango wa kwenda Simba Sc kwa msimu ujao.

Simba sc mpaka sasa wanasita kutuma ofa kutokana na ukweli kwamba dau la shilingi bilioni 1.3 ni kubwa zaidi kwa klabu hiyo kuweza kuilipa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala