Connect with us

Makala

Yanga Sc Kupiga na Red Arrows

Mabingwa wa Zambia Red Arrows watacheza dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga katika Siku Mwananchi Jumapili Agosti 04, 2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga sc imetangaza hayo mapema hii leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo katika mtaa wa Jangwani Kariakoo jijini Dar es salaam ambapo leo usiku shamrashamra kuelekea mchezo huo zitaanza.

Red Arrows ndio mabingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA KAGAME CUP’ mwaka 2024 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwezi huu baada ya kufanikiwa kuifunga Apr ya Rwanda kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Kikosi cha Yanga sc kinatarajiwa kuwasili usiku ya kesho saa tisa usiku ambapo mapokezi makubwa ya mashabiki yamepangwa kufanyika kusherehekea ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo ya fainali ya michuano ya Toyota Cup.

“Yanga imemfunga Kaizer Chiefs mabao manne na mashabiki wa timu iliyofungwa walijaza uwanja. Naomba mashabiki wetu pia Jumapili mjitokeze kwa wingi kuiona Yanga iliyojengeka,” amesema Haji Manara akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo

“Ni aibu kwa wanayanga kushindwa kuujaza uwanja wa Mkapa licha ya kuwa na kikosi bora ambacho kimejengwa na uongozi sambamba na benchi la ufundi kwa ajili ya kutoa raha kwa wananchi.”Alimalizia kwa kusema Manara ambaye atakua anajihusisha na hamasa zaidi klabuni hapo.

Yanga sc inatarajiwa kucheza mchezo huo utakaoambatana na shughuli nyingi za nje ya uwanja ili kukamilisha wiki ya mwananchi ambayo kilele chake ni Augusti 4 siku ya jumapili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala