Connect with us

Makala

Tepsie Kusalia Azam Fc mpaka 2026

Klabu ya Azam Fc imeamua kumuongezea mkataba mchezaji wake Tepsie Evance kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026 baada ya kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja katika ule wa awali uliokua unaisha mwaka 2025.

Tepsie ambaye ni zao halisi la akademi ya klabu hiyo amerejea klabuni hapo msimu huu baada ya kumaliza muda wake wa mkopo katika klabu ya Manispaa ya Kinondoni (Kmc) ambapo pamoja na kutopata muda wa kutosha wa kucheza bado mara kadhaa alipopata nafasi alionyesha kiwango kizuri.

Msimu huu Tepsia ana wakati mgumu wa kuhakikisha anapata nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na eneo analocheza la winga wa kulia ama kushoto sambamba na eneo la ushambuliaji wa pili kuwa na mastaa wengi kutoka nje ya nchi.

Eneo la kiungo wa ushambuliaji la Azam Fc msimu huu kuna maingiza mapya kadhaa wakiwemo Cheikna Diakite,Frank Tiesse,Nassor Saadun huku wakiungana na Gibril Sillah na Idd Nado waliokuwepo tangu msimu uliopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala