Connect with us

Makala

Job,Samata Watemwa Stars

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Hemed Morocco ametangaza kikosi  cha Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kitakachokwenda Nchini Azerbaijan kwaajili ya Michezo ya FIFA Series 2024 itakayofanyika wakati wa mapumziko ya kalenda ya Fifa ambapo amewatema baadhi ya mastaa waliokwenda Afcon.

Katika kikosi hiki aliyekosekana ni Mbwana Samatta, Mzamiru Yassin na Metacha Mnata ambao walikuwepo kwenye kikosi kilichocheza AFCON 2023 Ivory Coast huku Dickoson Job na Nickson Kibabage naye akikosena na wachezaji waliongezwa kikosi humo ni Clement Mzize na Yahya Zaydi.

Kukosekana na wahcezaji hao hasa Job kumewaibua wadau wengi wa soka nchini wakihoji kutokana na kiwango bora kabisa cha beki huyo licha ya walioitwa nao kuwa na ubora mkubwa.

Stars itakua na kazi ya ziada kufanya vizuri katika michuano hiyo mifupi baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Afcon 2023 nchini Ivory Coast ambapo ilitolewa katika hatua za awali.

Katika michuano hiyo Stars itamenyana na timu za Azerbaijan,Mongolia na Bulgaria ambao wako katika kundi moja ambao watacheza michezo hiyo ya kirafiki kuanzia machi 18-26 mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala