Connect with us

Soka

Feisal Kinara Ligi Kuu

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Azam Fc Feisal Salum amekua kinara wa ufungaji wa mabao katika ligi kuu ya Nbc msimu mpaka sasa baada ya kufanikiwa kufunga mabao 11 katika michezo 19 aliyocheza na timu yake ya Azam Fc.

Katika mchezo wa Dodoma Jiji mchezaji huyo alifunga mabao mawili dakika za 63 na 64 na kufikisha idadi hiyo ya mabao akimpita kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki aliyefunga mabao 10 mpaka sasa licha ya kukosa zaidi ya michezo mitatu ya mwanzoni mwa ligi kuu iliyokua imesimama kutokana na kupisha michuano ya Afcon mwezi Januari.

Wengine walioko kwenye orodha ya ufungaji bora mpaka sasa ni Maxi Nzengeli wa Yanga sc mwenye mabao nane na aliyekua mshambuliaji wa Simba sc Jean Baleke ambaye ana mabao nane pia sambamba na Waziri Junior wa Kmc na Marouf Tchakei wa Ihefu Fc.

Msimu uliopita Feisal akiwa Yanga sc alifanikiwa kufunga mabao sita na kutoa pasi tatu za magoli kwa nusu msimu aliocheza lakini sasa akiwa na klabu yake ya Azam Fc amejipata akifunga idadi hiyo ya mabao huku ikiwa bado msimu unaendelea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka