Connect with us

Soka

Azam Fc Yaifikia Yanga sc

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Dodoma Jiji Fc sasa klabu ya Azam Fc imefanikiwa kufikisha alama 43 sawa na Yanga sc katika msimamo wa ligi kuu nchini ambapo sasa timu zote zimefikisha alama 43 katika msimamo wa ligi kuu nchini.

Azam Fc ilipata ushindi huo katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam ambapo Ayoub Lyanga alianza kuandika bao la kwanza dakika ya 27 akiunganisha kwa kichwa pasi safi ya Iddi Nado huku pia Feisal Salum akifunga mabao mawili dakika za 63 na 64 na kufikisha jumla ya mabao 11 msimu huu.

Kipre Junior alihitimisha kalamu ya mabao kwa Azam Fc akifunga bao la nne dakika ya 69 ya mchezo huo ambao Dodoma Jiji Fc waliamua kujiachia kutunishiana misuli na Azam Fc baada ya kuwa na nidhamu ndogo ya ulinzi.

Emmanuel Martini aliipatia Dodoma Jiji Fc bao la kufutia machozi kwa penati dakika ya 84 ya mchezo baada ya mwamuzi kuwazadia penati kufuatia Hassan Mwaterema kuangushwa ndani ya boksi na Yanick Bangala.

Licha ya Azam Fc kuizidi Yanga sc michezo mitatu bado wameshindwa kuishusha kileleni kutokana na kuwa na wastani mdogo wa mabao ya kufunga na kufungwa huku Dodoma Jiji Fc baada ya kipigo hicho kikali wamesalia nafasi ya 12 ya msimamo wakiwa na alama 20 katika michezo 18 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka