Connect with us

Soka

Yanga Sc Kukutana na Hawa Robo Fainali Caf

Klabu ya Yanga sc imekubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Al Ahly Fc na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kupitia kundi D ikiwa kama mshindi wa pili baada ya dakika 90 za mchezo huo wa mwisho wa kundi hilo.

Yanga sc ilikubali bao hilo lilifungwa na Hussein Al Shahat dakika ya 46 ya mchezo huku pia upande wa pili Medeama Fc ikikubali kipigo cha 3-0 kutoka kwa Belouzdad lakini mchezo huo ulikua kukamilisha ratiba baada ya Yanga sc kufuzu kufuatia kumfunga Belouzdad mabao 4-0 hapa nchini.

Kutokana na kufanikiwa kufuzu kama mshindi wa pili klabu ya Yanga sc inaweza kukutana na timu za Mamelod Sundowns,Petro de Luanda ama Asec Mimosas ambazo zote zimemaliza kinara katika makundi yao ambapo Caf inatarajiwa kutangaza siku ya kufanyika kwa droo hiyo hivi karibuni.

Yanga sc haiwezi kukutana na Al Ahly kutokana na timu zote hizo kutoka kundi moja kwa mujibu wa kanuni za Caf pia haiwezi kukutana na timu za Simba sc,Tp Mazembe,Esperance kutokana na timu hizo kufuzu kama washindi wa pili katika makundi yao.

Michezo ya hatua ya robo fainali inatarajiwa kufanyika kati ya machi 29-31 baada ya droo rasmi kupangwa na Caf ambapo hivi karibuni kila timu itafahamu inakutana na nani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka