Connect with us

Soka

Rasmi Ihefu Yahamia Singida

Klabu ya soka ya Ihefu Fc ambayo imezoeleka kuwa na makazi yake mitaa ya Ubaruku Mbarali jijini Mbeya sasa imehamia mkoani Singida ambapo itatumia uwanja wa Liti kama uwanja wake wa nyumbani katika michezo ya ligi kuu ya Nbc inayoendelea nchini.

Baadhi ya wananchi wa mkoani Singida walishiriki kuipokea timu hiyo ambayo iliwasili rasmi jana mkoani humo kuja kuanza maisha mapya huku pia ikithibitika rasmi kuwa timu ya Singida Fountain Gate imehamia mkoani Mwanza ambapo itatumia uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wa nyumbani.

Leo watendaji wote wa timu za ligi kuu wametumiwa taarifa rasmi ya kuwa michezo yote ya nyumbani ya Ihefu SC itachezwa CCM Liti, Singida, Taarifa ya Bodi imesema kuwa Ihefu SC itatumia uwanja wa CCM Liti Singida badala ya HIGHLAND ESTATE, Ubaruku, Mbeya.

Hata hivyo tayari baadhi ya wachezaji wa Singida Big Stars walihamia Ihefu Fc wakati wa dirisha dogo wakimemo Elvis Rupia,Marouf Tchakei,Duke Abuya na Joash Onyango hivyo wanasingida watakua na sura ambazo wameshazizoea kuziona katika ligi kuu uwanjano hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka