Connect with us

Soka

Simba Sc,Azam Fc Hakuna Mbabe

Klabu za Simba sc na Azam Fc zimeshindwa kuamua nani mbabe baina yao baada ya kukubali sare ya 1-1 katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambao maelfu ya mashabiki kutoka kanda ya ziwa walihudhuria.

Azam Fc hawana budi kujilaumu wao wenyewe kutokana na kukosa nafasi nyingi katika mchezo huo licha ya kupata bao la mapema dakika ya 14 akimalizia pasi safi ya Pascal Msindo kutoka pembeni baada ya Azam Fc kufanya shambulizi la kushtukiza.

Prince Dube alikosa umakini mara na kushindwa kuweka mpira wavuni ambapo baada ya mapumziko kocha Abelhack Benchika alilazimika kumtoa Hussein Kazi na kuingia Kennedy Juma huku Fredy Michael akimpisha Pa Omar Jobe na Israel Mwenda akimpisha Shomari Kapombe hali iliyobadili mchezo.

Mabadiliko hayo yaliinufaisha Simba sc ambayo ilifanikiwa kusawazisha bao kwa faulo iliyopigwa na Cletous Chama dakika ya 90+3 na kuweka mzani sawa ambapo mpaka dakika zinaisha timu hizo ziligawana alama moja moja.

Kutokana na Sare hiyo Simba sc imefikisha alama 30 katika nafasi ya tatu ikiwa na michezo 13 huku Azam Fc imefikisha alama 32 ikiwa na michezo 14 huku Yanga sc akiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka