Connect with us

Soka

Kagera Sugar Yaikomalia Yanga Sc

Timu ya Kagera Sugar Fc imefanikiwa kulazimisha sare katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera ambapo mchezo ulimalizika kwa suluhu 0-0.

Yanga sc ilianza mchezo huo kwa kasi ambapo Yanga sc ilikua na mipango mizuri kuanzia nyuma mpaka katikati mwa uwanja lakini ilikosa mipango ndani ya eneo la hatari na kumfanya mshambuliaji Clement Mzize kuwa mzururaji.

Kagera Sugar walibaki wengi nyuma ya uwanja wakikaba zaidi lakini walipata nafasi kadhaa za kushambulia kwa kushtukiza lakini nao walikosa ufanisi mbele ya lango ambapo kipa wa Yanga sc Metacha Mnata aliokoa baadhi ya hatari.

Yanga sc walifanya mabadiliko wakiwaingiza Joseph Guede na Kennedy Musonda lengo likiwa ni kupata bao lakini mipango mingi ilizimwa na mabeki wa Kagera sugar huku Kipa Ramadhani Chalamanda akiokoa hatari kadhaa na kuliweka lango salama.

Baada ya dakika tisini kuisha Yanga sc walibaki na alama 31 katika nafasi ya pili ya msimamo huku Kagera Sugar wakiwa katika nafasi ya 13 wakiwa na alama 14.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka