Connect with us

Makala

Simba Sc,Chama Mambo Safi

Klabu ya Simba sc imeamua kumsamehe kiungo wake Cletous Chama baada ya kumsimamisha kwa muda kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu ambalo lilitokea mwaka jana kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Wydad Athletic Club uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Inadaiwa kuwa kiungo huyo alimtolea lugha chafu kocha msaidizi wa klabu hiyo wakati wa mazoezi ya kupasha mwili kuelekea mchezo huo ambapo taarifa kutoka klabuni hapo ilisema kuwa klabu hiyo imemsimamisha mchezaji huyo na kumpeleka kamati ya nidhamu ya klabu hiyo.

Leo klabu hiyo imetoa taarifa iliyopokelewa kwa maoni tofauti ambapo klabu hiyo imeamua kumsamehe mchezaji huyo baada ya kuomba radhi tayari amesafiri kuelekea mkoani Kigoma kujiandaa na mchezo dhidi ya Mashujaa Fc utakaofanyika kesho katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Mkataba wa Chama na Simba sc unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu huu ambapo taarifa zinadai kuwa mabosi wa klabu hiyo wana mpango wa kuachana naye hasa wakipata mbadala sahihi wa nafasi yake klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala