Connect with us

Soka

Senegal Yatolewa Afcon 2024

Timu ya Taifa ya Senegal imetolewa katika michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-4 kwa penati dhidi ya timu ya Taifa ya Ivory Coast baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo wa kufuzu robo fainali.

Senegal ilikua ya kwanza kupata bao la mapema dakika ya nne kupitia kwa Habib Diallo aliyemalizia pasi nzuri kutoka kwa Sadio Mane ambapo bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 86 ya mchezo ambapo Frank Kessie alifanikiwa kufunga penati baada ya Kipa wa Senegal Eduardo Mendy kumuangusha mshambuliaji wa Ivory Coast ndani ya eneo la hatari.

Baada ya dakika tisini na mwamuzi kuamua kuongeza dakika 120 bado matokeo yalibaki 1-1 ambapo kwa mujibu wa sheria aliamuru mikwaju mittano ya penati ambapo Ivory Coast walipata penati 5 huku Senegal wakipata penati 4 ambapo Kalifa Coulibaly alikosa penati yake.

Ivory Coast sasa wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ambapo watakutana na Cape Verde katika hatua hiyo huku wakiwa na kazi ngumu ya kufanya kupata ushindi kutokana na kutoanza vizuri katika michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka