Connect with us

Soka

Diarra Aipa Alama 3 Mali

Kipa wa klabu ya Yanga sc Djigui Diarra amefanikiwa kuisaidia timu ya Taifa ya Mali kupata alama tatu katika mchezo wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2024) dhidi ya Afrika ya Kusini uliofanyika katika uwanja wa  Amadou Gon Coulibaly.

Katika mchezo huo kipa huyo alianza katika kikosi cha kwanza ambapo alifanikiwa mara kadhaa kuwaweka mchezoni mastaa wa timu hiyo akiokoa michomo mikali iliyopigwa golini na washambuliaji wa Afrika Kusini wakiongozwa na Percy Tau.

Mali kutokana na kupata alama hizo tatu muhimu kupitia mabao ya Hamari Traore dakika ya 60 na Lassine Sinayoko dakika ya 66 ambapo sasa wapo kileleni mwa kundi E wakiwa na alama 3 sambamba na Namibia huku Afrika kusini na Tunisia wakiwa hawana alama.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka