Connect with us

Soka

Mbombo Atua Nkana Fc

Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, Idriss Mbombo amejiunga na klabu ya Nkana FC ya Zambia na kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa klabu hiyo kwa mkataba ambao haukuwekwa wazi na kutambulishwa siku ya ijumaa na Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Kelvin Mutafu.

Mshambuliaji huyo aliomba kuvunja mkataba wake ambao ulisalia na klabu ya Azam FC ili awe mchezaji huru ambapo muda mchache alisafiri haraka kwenda nchini Zambia kujiunga na Nkana ambapo alijumuika na mastaa wengine watatu katika utambulisho huo.

Mshambuliaji huyo ameondoka Azam Fc baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza ambapo kocha Yousouph Dabo anapenda zaidi kumtumia Prince Dube kama mshambuliaji wake wa kati huku akisaidiwa na Allasane Diara na mara nyingi Mbombo hukaa jukwaani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka