Connect with us

Soka

Yanga Sc Vs Kvz Hakuna Mbabe

Klabu ya Yanga sc imeshindwa kuibuka na alama tatu katika mchezo wa kombe la Mapinduzi wa Kundi C dhidi ya Kvz uliofanyika katika uwanja wa Amani Visiwani humo baada ya kulazimishwa suluhu katika dakika tisini za mchezo huo.

Kocha Miguel Gamond aliamua kuanza na vijana kutoka kikosi B huku akiwachanganya na wakongwe kama Jonas Mkude,Crispine Ngushi,Dennis Nkane ambapo vijana hao walijitahidi kupambana katika dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo matokeo mpaka mapumziko yalikua 0-0.

Kvz hawana budi kujilaumu wenyewe kutokana na kukosa utulivu hasa katika eneo la umaliziaji licha ya kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga mabao.

Kipindi cha pili Yanga Sc waliamua kuingiza wachezaji wazoefu akiwemo Kibwana Shomari,Jesus Moloko,Farid Musa huku usajili mpya Augustine Okrah akiumia dakika chache tu baada ya kuingia.

Mpaka dakika tisini zinakamilika timu hizi zilitoka suluhu huku zote zikifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ambapo timu mbili kutoka kila kundi zimefuzu huku Jamhuri Fc ikitolewa katika michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka