Bosi wa klabu ya Yanga sc Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ amenunua tiketi zote za mzunguko kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Medeama itakayopigwa Jumatano ijayo Uwanja wa Mkapa baada ya mechi ya awali kumalizika kwa sare ya bao 1-1 mjini Kumasi, Ghana.
Hayo yamethibitishwa na msemaji wa klabu hiyo Ali Kamwe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu tukio hilo ambapo aliibatiza rasmi kuwa siku hiyo itaitwa “Gsm Day” ili kuthamini mchango wa tajiri huyo katika klabu hiyo.
“Tumekuwa na kawaida ya kuwa na siku za wachezaji, sasa tumekuja kiutofauti, mdhamini na mfadhili wetu Ghalib Said Mohamed amenunua tiketi zote za mzunguko. Hivyo mechi ya Medeama FC tunakwenda kwa jina la GSM Day kuthamini mchango wake kwenye mchezo huu” Alisema Ally Kamwe
Kuhusu namna ya mavazi kama ilivyokawaida katika siku hizo maalumu za klabu hiyo Ali Kamwe alisema Ili kuheshimisha siku ya tajiri? Namna pekee ya kumuonesha tunathamini mchango wa GSM, siku ya jumatano hakikisha unakuja na jezi ambayo imetengenezaa na GSM. Ukija na jezi chupli hutaruhusiwa kuingia uwanjani.”
Yanga sc itakua na wakati mgumu kupambana na presha itakapo wakaribisha Medeama Fc katika mchezo huo siku ya Jumatano ambapo ushindi pekee ndio utatoa matumaini ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.