Connect with us

Soka

Wababe Cecafa Kukutana Mapinduzi Cup

Michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza kutimua kivumbi, Desemba 28 mwaka huu kwenye Dimba la Amaan Zanzibar huku timu kumi na nne zikiwemo mbili za Tanzania bara zikitarajiwa kushiriki michuano hiyo yenye lengo la kutunza historia ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa ZFF akiweka wazi mambo muhimu kuhusu michuano hiyo ikiwa ni pamoja na kutaja timu 12 zitakazoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Disemba 28 mpaka Januari 13 ambapo timu za Mlandege, KVZ, Jamuhuri na Chipukizi kwa upande wa Zanzibar na timu ya Azam, Simba, Singida Fountain Gate na Yanga kutoka Tanzania Bara.

Ameongeza kuwa katika kuendeleza ujirani mwema wa kimichezo wamezialika Timu ya URA kutoka Uganda, Bandari kutoka Kenya na APR ya Rwanda pia amesema mashindano hayo yatachezwa katika Uwanja wa Amani, hivyo wananchi watarajie michuano yenye mvuto kulingana na ubora wa uwanja huo.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya Mlandege iliyotwaa ubingwa huo baada ya kushinda magoli 2 -1 dhidi ya Singida Big Stars, ikiwa wote ni fainali yao ya kwanza ya kombe hilo ambalo ni maalumu kwaajili ya kuazimisha Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka