Klabu ya Simba sc imerejea nchini ikiwa na matumaini kibao ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika licha ya kuwa mkiani mwa kundi B ikiwa na alama mbili mpaka sasa baada ya kufungwa 1-0 na Wydad Athletics Club ya nchini Morroco.
Simba sc iliruhusu bao la dakika za mwishoni mwa mchezo licha ya kucheza vizuri mchezo huo uliochezwa katika uwanja mgumu wa Stade de Marrakech uliopo nchini humo huku kukiwa na mashabiki wa nguvu waliokua wakiwasapoti wenyeji.
Simba sc inajipanga kwa ajili ya mchezo wa marejeano dhidi ya Wydad utakaofanyika nchini siku ya Disemba 19 ambapo anapaswa ashinde mchezo huo ili kujiwekea matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.
Licha ya kufungwa mchezo hup kocha wa timu hiyo Abelhad Benchika alionyesha kuvutiwa na kiwango cha timu hiyo wakati wote wa mchezo huo.
“Yote yaliyotokea hapa yatakwenda kutupa usahihi wa maandalizi mazuri ya mchezo ujao. Eneo tulilokuwa bora tutakwenda kuongeza ili kuimarika zaidi na kwenye mapungufu tutakwenda kuparekebisha.” Alisema Kocha Benchikha.
Simba sc mpaka sasa ina alama mbili katika kundi B huku Asec Mimosa akiongoza kundi hilo akiwa na alama saba huku Janweng Galaxy akiwa na alama nne na Wydad akiwa na alama tatu.