Connect with us

Soka

Mayele Apenya Afrika

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele ambaye kwasasa anakipiga Pyramids Fc ya nchini Misri ameingia tatu bora katika tuzo ya mchezaji wa mashindani CAF akiburuzana na staa wa Al Ahly, Percy Tau na Petter Shalulile anayekiwasha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Staa huyo raia wa Congo DRC amefanikiwa kuingia tatu bora baada ya kuwa na msimu mzuri uliopita alipokua akikipiga kunako klabu ya Yanga sc ambapo alikua mfungaji bora wa kombe la Shirikisho barani Afrika huku akiiwezesha Yanga sc kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Tuzo hizo zitatolewa Desemba 11 nchini Morocco ambapo japo uwezekano wa staa huyo kushinda ni mdogo lakini kuingia katika hatua hiyo kunaleta matumaini kuwa lolote linaweza kutokea kutokana na kuonyesha kiwango hicho kilichoivutia Pyramids Fc kutoka zaidi ya bilioni mbili kumnasa staa huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka