Connect with us

Soka

Wawa Aiponza Singida FG

Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate Fc  imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Pascal Serge Wawa ambaye ilimtema mwanzoni mwa msimu huu bila kufuata utaratibu na kusababisha mchezaji huyo kushtaki Fifa.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikkisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Wawa kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Klabu hiyo ambapo ilitakiwa imlipe ndani ya muda wa siku 45 tangu uamuzi huo utolewa lakini klabu hiyo haikufanya hivyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo ni kwamba mchezaji huyo raia wa Ivory Coast alifungua kesi FIFA alidai malipo ya ada ya usajili (sign on fee) na malimbikizo ya mishahara wa muda ambao haukuwekwa wazi hivyo Fifa baada ya kupitia vielezo iliamuru mara moja klabu hiyo kumlipa ndani ya siku 45 ambapo amri hiyo haikutekelezwa hivyo klabu sasa rasmi imefungiwa kusajili mpaka imlipe staa huyo wa zamani wa Azam Fc na Simba sc.
Kutokana na hilo Fifa imeaifungia klabu hiyo kusajili wachezaji wa kimataifa kuanzia sasa huku Shirikisho la soka nchini limeifungia klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wa ndani mpaka pale itakapokamilisha kulipa deni hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka