Connect with us

Soka

Chasambi Azitoa Jasho Simba Sc,Yanga Sc

Klabu za Simba sc na Yanga sc zimeendelea kutoana jasho kuwania saini ya kinda wa klabu ya Mtibwa Sugar Ladack Chasambi ili ajiunge nazo katika usajili wa dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Taarifa za ndani zinasema kuwa timu hizo zote zinapambana ili ziweze kumsajili kinda huyo ambaye amebakiza mkataba wa miaka miwili klabuni hapo ambapo klabu zote mbili mbili ziko tayari kuvunja mkataba huo ili kumpata mchezaji huo bora wa ligi ya vijana ya chini ya umri wa miaka 20.

Simba sc wapo mbele katika kuinasa saini ya mchezaji huyo dili ambayo pia hata mchezaji mwenyewe akionekana kuikubali ambapo atasaini mkataba wa miaka mitatu huku akiona kama ana uhakika wa kucheza tofauti na Yanga sc ambao wamempa mkataba mnono wa miaka miwili huku kukiwa na mshahara mkubwa kuliko ule wa Simba sc japo changamoto kubwa ni upatikanaji wa nafasi ya kucheza kutokana na klabu hiyo kuwa na mastaa wa maana.

Mpaka sasa bado uongozi wa mchezaji huyo unajadiliana nae kuona wapi aelekee kwa maslahi mapana ya kupata fedha pamoja na kulinda kipaji cha mchezaji husika ambaye anataka kucheza mara kwa mara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka