Connect with us

Soka

Kagere Atupia Dhidi ya Coastal

Timu ya Singida Fountain Gate imefanikiwa kupata alama tatu ikiwa uwanja wake wa nyumbani wa Liti mkoani Singida baada ya  kushinda mabao 2-1 ikicheza na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Singida ikiingia kwa kujiamini kama mwenyeji ilipata bao la kwanza likifungwa na Meddie Kagere dakika ya 30 huku akiacha ujumbe ‘Mnafiki ishi nae kinafiki’ na bao la pili Felly Mulumba akijifunga dakika ya 52 huku Bao la Coastal likiwa limefungwa na Maabad Maulid dakika ya 72.

Sasa Singida FG imefanikiwa kufikisha alama kumi na nane ikipanda mpaka nafasi ya nne ya msimamo huku Coastal union ikishuka mpaka nafasi ya kumi na mbili ikiwa na alama kumi huku timu zote zikiwa zimecheza michezo kumi na moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka