Connect with us

Soka

Yanga Sc Kurejea Kwa Kishindo

Baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa CR Belouzdad ya nchini Algeria katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika sasa klabu hiyo inajipanga kurudi upya katika michuano hiyo.

Yanga sc tayari imewasili nchini kujiandaa na mchezo wa pili utakaofanyika Disemba 2 katika uwanja wa Benjamini Mkapa dhidi ya Al Ahly Fc majira ya saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

Katika mchezo uliopita licha ya kumiliki sana mpira ugenini bado klabu hiyo haikua na umakini hasa kuzuia pindi inapopoteza mpira huku nusu ya wachezaji wakiwa tayari katika nusu ya wapinzani.

Kocha Miguel Gamond ana kazi kubwa ya kufanya kuelekea mchezo huo mkubwa dhidi ya klabu kubwa barani Afrika huku akichukua funzo kutoka katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Belouzdad.

“Tulifanya makosa makubwa matatu, nadhani ndio hayo ambayo yamewapa ushindi wenzetu, ni makosa ya kushindwa kucheza kwa nidhamu ya mchezo, hayo ndiyo matokeo ya soka wakati mwingine unaweza kucheza vizuri lakini matokeo akapata mpinzani,” Alisema kocha Gamond akielezea kuhusu mchezo huo dhidi ya Belouzdad

“Hatuna muda wa kupoteza, tunarudi kujiandaa na mchezo ujao, tutakwenda kukutana na timu nyingine bora, hatuna budi kusahau yote ya mchezo huu kwani ile ni mechi nyingine dhidi ya timu nyingine.

Yanga Sc wanahitaji kushinda katika mchezo huo dhidi ya Al Ahly ili kupata uhakika wa kumaliza katika nafasi mbili za juu katika kundi D la michuano hiyo mikubwa barani Afrika ili kufuzu hatua ya robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka