Connect with us

Soka

Simba Sc Wafungiwa na Fifa

Klabu ya Simba imefungiwa kusajili na shirikisho la soka Duniani (Fifa) mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mauzo ya mchezaji Pape Sakho yaliyofanyika wakati wa dirisha kubwa la usajili.
Uamuzi huo umefanywa na Fifa na kutangazwa na Shirikisho la soka nchini (TFF) mara baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya nyota huyo ambapo Simba sc walipewa siku arobaini na tano wawe wamelipa fedha hizo.
Kwa mujibu wa makubaliano baina ya vilabu hivyo wakati wa mauziano ya mchezaji huyo kuliwekwa kipengele cha asilimia ya fedha ambapo klabu hiyo itapata endapo nyota huyo atauzwa kwenda klabu nyingine ambapo alizwa kwenda klabu ya Quevilly Rouen Metropole ya nchini Ufaransa.
Kutokana na adhabu hiyo pia TFF imeifungia klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wa ndani kama ilivyo adhabu ya Fifa ya kuzuiwa kufanya usajili wa wachezaji wa nje ya nchi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka