Connect with us

Soka

Simba Sc,Yanga Sc Zapiga Hodi Mtibwa Sugar

Klabu za Simba sc na Yanga sc kwa pamoja zimepiga hodi katika klabu Ya Mtibwa Sugar zikihitaji saini ya kinda Ladack Chasambi ili ajiunge na klabu hizo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Kinda huyo aliyenzia timu ya vijana ya Mtibwa Sugar amegeuka lulu katika ligi kuu nchini kutokana na uwezo wake uwanjani akiwa anaweza kucheza kama winga wa kulia na kushoto pamoja na mshambuliaji wa pili wa kati (Namba 10).

Mtendaji mkuu wa Mtibwa Sugar Fc Swabri Mohamed amesema kuwa tayari kuna baadh ya timu za ligi kuu nchini zimeonyesha nia ya kumsaini kinda huyo huku tayari timu hizo zimeshatajiwa bei.

“Simba na Yanga wote wamegonga hodi Mtibwa Sugar kutaka kumsajili Ladack Chasambi. Tumeshawatajia dau la mchezaji wetu mwenye mkataba, kwahiyo wajipange waje mezani tumalizane.” Alisema Swabri ambaye ndie bosi wa Mtibwa Sugar Fc.

Mtibwa Sugar Fc imekua na kawaida ya kunyanyua vipaji vingi mkoani Morogoro ambapo mastaa kama Mzamiru Yassin,Dickson Job,Kibwana Shomari na wengineo wametokea katika klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka