Connect with us

Soka

Kmc Kujipima kwa Al Hilal Fc

Wakati kikosi cha Al Hilal Fc kikiwa hapa nchini kujiandaa na michuano ya kimataifa kesho kinatarajiwa kukutana na Kmc Fc kucheza mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Baobab uliopo mjini Bagamoyo.

Al Hilal Fc ikiwa chini ya kocha Florent Ibenge imechagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wa nyumbani katika michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika hatua ya makundi hivyo kuwalazimu kuweka kambi hapa nchini.

Kmc itafaidika na mchezo huo kutokana na kwamba timu hiyo kwa sasa ipo katika maandalizi kutokana na ligi kusimama kupisha kalenda ya Fifa ya michuano ya kufuzu kombe la dunia kwa timu za Taifa mwaka 2026.

Kocha Mkuu wa KMC, Abdihamid Moallin amesema “Ligi kwa sasa imesimama, tumeendelea na maandalizi kwani kwaajili ya mechi zijazo.

Tulihitaji mechi za kirafiki na kwa bahati nzuri tumeipata Hilal moja ya timu bora Afrika na tutashirikiana nao

“Pamoja na yote tutacheza mechi ya kirafiki itakayotupa tathimini ya kikosi chetu kabla ya kuendelea na ligi tutakapocheza na Kagera.”Alisema Moalin aliyeifundisha Azam Fc kabla ya kutua Kmc.

Kmc itautumia mchezo huo kwa  maandalizi ya mechi ijayo ya ligi dhidi ya Kagera Sugar kwa huku kwa Hilal ikiwa ni maandalizi ya mechi ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda, Novemba 25.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka