Connect with us

Makala

Robertinho Atimuliwa Simba sc

Klabu ya Simba sc imetangaza kuachana na kocha Roberto Oliveira “Robertinho” ikiwa ni siku mbili baada ya kupokea kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa watani zao Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imesema kuwa kocha huyo ametimuliwa pamoja na kocha wake wa viungo Corneille Hategimana huku nafasi hiyo ikizibwa kwa muda na kocha wa makipa Dani Cadena atakayesaidiwa na Seleman Matola.

Robertinho amekuwa kwenye shinikizo muda wote aliokuwa kwenye klabu hiyo bila kujali matokeo mazuri ambayo amekuwa akitapata kwenye ligi ambapo tangu awasili klabuni hapo ameiongoza timu hiyo katika michezo 18 akishinda 15 sare michezo 2 na kufungwa mchezo mmoja.

Pengine suala la kufukuzwa kwa kocha Robertinho linatokana na timu hiyo kutocheza vizuri mbali na matokeo mbalimbali anayopata huku safu ya ulinzi ikiruhusu magoli mengi ya kizembe hata katika mechi ndogo kama dhidi ya Mtibwa Sugar na Ihefu Fc.

Taarifa za kufukuzwa kwa kocha huyo zimekua na mgawanyiko miongoni wa wadau wa soka nchini ambapo wengi wamekua wakihoji kuhusu kufukuzwa kwake licha ya kuwa na takwimu nzuri katika ligi kuu hasa msimu huu ambapo katika michezo saba waliyocheza Simba sc mpaka sasa wamefungwa mmoja pekee huku wakiwa wameshinda michezo sita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala