Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuifunga Azam Fc kwa mabao 3-2 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo uliokua mzuri na wa kuvutia wenye hadhi ya ligi kuu ambapo mastaa Feisal Salum,Prince Dube,James Akaminko,Sospeter Bajana walishindana katika eneo la katikati na Khalid Aucho,Mudathir Yahaya na Pacome Zouzou pamoja na Aziz Ki.
Iliwachukua Yanga sc dakika nane tu kupata bao la uongozi kupitia kwa Stephane Aziz Ki aliyetumia akili binafsi kufunga bao mbele ya mabeki wa Azam Fc ambao walietegeana kuokoa mpira ambao ulionekana kama hauna madhara.
Azam Fc walisawazisha bao hilo dakika ya 18 kupitia kwa Gibri Sillah ambaye aliachia shuti kali nje ya box ambalo lilimshinda kipa Djigui Diarra huku mabeki ya Yanga sc wakibaki wanashangaa ambapo Sillah tena aligeuka mwiba baada ya kumzidi maarifa nahodha Bakari Mwamnyeto ambaye alimuangusha na mwamuzi kuweka penati iliyofungwa vizuri na Prince Dube dakika ya 62.
Bao hilo halikudumu kwani Aziz Ki alimtungua kipaAbdulai Iddrisu kwa shuti kali la faulo ambalo lilimshinda na kujaa wavuni dakika ya 69 huku dakika tatu baadae Aziz Ki tena alifunga bao la tatu kwake na kwa timu yake akitumia vyema makosa ya mabeki wa Azam Fc.
Kutokana na ushindi huo sasa Yanga sc imerejea kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 15 katika michezo sita huku Simba sc ikiwa katika nafasi ya pili na alama 15 ikizidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa na Azam Fc wapo katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini.