Connect with us

Makala

Mwakinyo Afungiwa Mwaka 1

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Hassan Mwakinyo amefungiwa mwaka mmoja kushiriki mapambano mbalimbali ya ngumi ndani na nje ya nchi kutokana na kosa la kususia pambano dhidi ya Julius Idongo siku ya Septemba 29.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (TPBRC) George Lukindo amesema kuwa mbali na adhabu hiyo Mwakinyo anatakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni Moja kwa shirikisho hilo kutokana na kutenda kosa hilo ambapo pia alitoa lugha isiyo na staha wakati wa kikao na shirikisho hilo.

Adhabu ya Mwakinyo inaanza leo Okroba 10, 2023 hadi Oktoba 10, 2024 ambapo hatakiwi kushiriki pambano lolote rasmi ndani na nje ya nchi.
“Nilielewa sana huu mchezo mchafu,nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatima iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa,nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili ili inapotokea inshu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu”.
“Ni kweli pesa inaweza kununua haki na utu wa mtu lakini hiyo ni kwa mtu boya asiyejua thamani na haki zake za msingi..see you very soon”Ulisomeka ujumbe wa Bondia Mwakinyo siku moja kabla ya uamuzi wa shirikisho hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala