Connect with us

Makala

Bajana Mambo Magumu Azam Fc

Kiungo wa Azam Fc Sospeter Bajana amekua na wakati mgumu klabu hapo baada ya kutovaa kitambaa cha unahodha katika michezo ya hivi karibuni huku akianzia benchi mara kadhaa kutokana na kutopangwa na kocha Yousouph Dabo.

Kwenye michezo ya hivi karibuni mambo yamekuwa tofauti kidogo kwenye eneo la unahodha wa Azam FC,Mchezo dhidi ya Singida Big stars Bajana alianzia benchi na Amoah alionekana akiwa na kitambaa cha unahodha.Lakini baada ya Bajana kuingia mchezoni Amoah hakumkabidhi kitambaa Bajana kama ambavyo huzoeleka.

Kwenye mchezo dhidi ya Dodoma jiji Amoah na Bajana wote walianza kwenye mchezo huo na Amoah ndiye alionekana amevaa kutambaa cha unahodha kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Bajana amekuwa na wakati mgumu tangu arejee kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa mwezi uliopita na taarifa zinaeleza kuwa amekwaruzana na Kocha wake Youssouph Dabo (Mwanaspoti wameripoti) jambo ambalo limefanya hata nafasi yake ya kuanza kwenye kikosi kuwa finyu na hata kupoteza nafasi yake ya unahodha kikosini hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala