Connect with us

Makala

Yanga sc Yafuzu Makundi Kibabe

Hatimaye baada ya miaka 25 kupita klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika tangu ifanye hivyo mwaka 1998 baada ya kuingia hatua ya nane bora kwa kipindi hicho.

Yanga sc imekata mwiko huo kibabe baada ya kufanikiwa kuitoa timu ngumu ya Al Merrekh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0 ikishinda 2-0 ugenini nchini Rwanda katika uwanja wa Pele ambapo klabu hiyo ilichagua kutumia kama uwanja wa nyumbani kutokana na machafuko ya kisiasa nchini mwao.

Pia katika mchezo wa marudiano siku ya Jumamosi Yanga sc ilishinda tena kwa bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi na kukata tiketi hiyo muhimu sana msimu huu.

Licha ya kuwa na umiliki mkubwa wa mpira iliwalazimu Yanga sc kumsubiri Clement Mzize aliyeingia kipindi cha pili ili kuja kupata bao pekee la mchezo huo dakika ya 66 ya mchezo huku Nyota Stephane Aziz Ki akikosa mabao kadhaa ya wazi.

Sasa Yanga sc itasubiri mpaka siku ya ijumaa ili kujua itakutana na nani katika hatua ya makundi baada ya kuwekwa poti namba tatu ambapo yupo na timu za TP Mazembe (23),Yanga SC (21),Asec Mimosas (20),Al Hilal (20.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala