Connect with us

Makala

Inonga Nje Wiki Moja

Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba sc Henock Inonga huenda akakaa nje akiuguza majeraha takribani wiki moja na nusu akiuguza kidonda ambacho alipata kwenye mchezo wa ligi kuu Simba sc ilipocheza dhidi ya Coastal Union.

Daktari wa timu anasema Inonga anaendelea kupata matibabu na anaendelea vizuri lakini atalazimika kukaa nje takribani wiki moja na nusu ili kuruhusu mshono ushike vizuri na kidonda kupona kabisa.

“Ni kidonda kikubwa ambacho kimemuuza na kupata hitilafu katika mguu wake hivyo tunamfanyia Dressing na kumpa antibiotic ili aweze kurejea na pengine inaweza kuchukua wiki moja au moja na nusu ndio anaweza kuanza mazoezi”Alisema Edwin Kagabo ambaye ni Daktari wa klabu hiyo.

Inonga alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambapo alikanyagwa vibaya mguuni na kiungo wa timu hiyo Hija Ugando na kulazimika kukimbizwa hospitali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala