Connect with us

Makala

Usajili Mpya Waiokoa Singida FG

Usajili mpya wa mshambuliaji raia wa Kenya Elvis Rupia umeanza kulipa baada ya kufanikiwa kufunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika baina ya timu hiyo na Future Fc ya nchini Misri.

Bao hilo la dakika ya 53 limeipa matumaini Singida Fountan Gate ambayo itaelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano na klabu hiyo baada ya wiki mbili ambapo mshindi ataingia moja kwa moja hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kocha Ernst Middendorp aliamua kuanza na maingizo mapya kikosini humo akiwaanzisha Gadiel Michael kama kiungo huku beki Hamad Waziri akianza badala ya Joash Onyango huku pia akimtambulisha Bruno Gomez kama namba kumi akisaidia na Tchakei.

Singida Fountain Gate inabidi wajipange vilivyokuelekea mchezo wa marudiano nchini Misri ikizingatiwa kuwa nchini hizo zinajulikana kwa fitna za soka hasa pale kwenye michezo ya hatua za mtoano ambapo klabu hizo hujua namna ya kuzicheza ili kutimiza malengo huku pia ugeni wa Singida katika anga za kimataifa pia inaweza kuwa kikwazo kwao japo mastaa wengi wa timu hiyo wana uzoefu na michuano hiyo kwa maana walishacheza mechi hizo wakiwa na klabu zingine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala