Connect with us

Makala

Mashabiki Yanga sc Wafunika Kigali

Zaidi ya mashabiki elfu moja wa klabu ya Yanga sc wamewasili nchini Rwanda kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Al Marreikh ya nchini Sudan ambao utafanyika Septemba 16 katika uwanja wa Pele Nyamirambi jijini Kigali.

Ikiwa tayari msafara wa wachezaji na viongozi wa klabu hiyo uliwasioi tangu jana jioni mapema asubuhi ya leo msafara wa mashabiki wa klabu hiyo waliokua katika mabasi zaidi ya 20 uliwasili eneo la Rusumo ulipo mpaka wa Tanzania na Rwanda na baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji msafara huo uliingia jijini Kigali.

Msafara huo ulipokelewa na Rais wa Yanga sc Eng.Hersi Said pamoja na makamu wa Rais wa klabu hiyo Arafat Haji ambapo moja kwa moja waliwashukuru mashabiki hao kwa moyo wao huo wa kupambania timu hiyo huku raia wengi wa nchi hiyo wakishangazwa na umati huo uliokua na shangwe la kutosha.

Msafara huo ni ule wa kwanza ambao ulianzia jijini Dar es salaam huku ikisemekana kuwa zaidi ya mabasi mengine 20 yanakuja kutokea mikoa ya kanda ya ziwa yakiwa yamejaza mashabiki wa kutosha.

Mwitikio wa mashabiki hao umekua wa kushangaza licha ya gharama kubwa za usafiri huku kiingilio pekee kikiwa ni Tsh 20000 ya Tanzania huku kwa wale wa Dar es salaam wakilipa takribani Tsh.150000 kama nauli pekee.

Yanga sc kesho wanaanza safari ya mechi mbili kuhakikisha wanafuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo mara ya mwisho walifuzu mwaka 1998.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala