Connect with us

Football

Majeraha Kikwazo Kiungo Simba Sc

Kiungo wa klabu ya Simba sc Aubin Kramo ameomba ruhusa ya kurejea nchini kwao Ivory Coast Kwa ajili ya kupata matibabu zaidi kutokana na kuandamwa na majeraha tangu ajiunge na kikosi hicho akitokea Asec Mimosa ya nchini kwao Ivory Coast.

Tangu ajiunge na kikosi hicho staa huyo hakua amecheza mchezo wowote rasmi huku baada ya kurejea mazoezini lakini aliumie tena ambapo wikiendi iliyopita kiungo huyo alijitonesha jeraha lake la goti kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome Fc.

Majeraha hayo sasa imesemekana kuwa yamemchanganya kiungo huyo kiasi cha kuamua kuomba ruhusa kurudi nyumbani kwao kwenda kujitibu zaidi ili akirudi awe amepona moja kwa moja na kuanza kukitumikia kikosi hicho.

Kocha Robertinho ameonekana kuvutiwa na kiwango cha kiungo huyo ambapo katika michezo ya kirafiki ya ambapo staa huyo alifanikiwa kufunga katika michezo hiyo.

Mpaka sasa bado uongozi wa klabu hiyo haujathibitisha endapo utamruhusu ama la utamtaka abaki nchini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kurudi fiti kabisa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Football