Connect with us

Makala

Pacome Amtisha Kocha El-Merrekh

Kocha wa El Merreikh ya Sudan Osama Nabieh amesema japokuwa Yanga ina wachezaji wengi wa kuchungwa ambao ni hatari ila akili yake na wachezaji wake ni namna ya kumzuia kiungo huyo ambaye kiwango chake anakifahamu tangu akiwa Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kocha huyo amesema hayo kuelekea mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Yanga sc utakaofanyika nchini Rwanda Septemba 16 ambapo El-Merrekh watakua wenyeji katika mchezo huo ulioteka hisia baada ya mashabiki wengi wa Yanga sc kujitokeza kusafiri na timu.

“Yanga Ina wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kupambana na timu yeyote ile ila Mimi kichwa kinaniuma jinsi ya kumzuia kiungo Pacome Zouzoua Kwa ninamfahamu tangu siku nyingi, japo tumejiandaa kupambana nao na kushinda mechi hii dhidi yao”.Alisema kocha huyo.

Yanga sc inatarajiwa kuifuata timu hiyo kuanzia Septemba 14 huku kocha Miguel Gamondi akiwa na wakati mgumu wa kuamua kikosi cha kwanza kutokana na umuhimu wa mchezo huo huku wachezaji wengi wa kikosi hicho wakionyesha kuwa wako tayari kwa mchezo hasa katika eneo la kiungo ambapo Pacome,Aziz Ki na Maxi Nzengeli wakishindani nani aanze nyuma ya mshambuliaji.

Msimu uliopita katika hatua kama hii Yanga sc ilitolewa na Al Hilal ya Sudan kwa jumla ya mabao 2-1 na kuangukia katika kombe la shirikisho ambapo walifika fainali lakini msimu huu utaratibu umebadilika na atakayefungwa atabakia kuwa mtazamaji tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala