Connect with us

Makala

Mastaa Yanga sc Wapelekwa Ufukweni

Kocha wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi amewashtua mastaa wa timu hiyo baada ya kuamua kuwapeleka kupiga mazoezi katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es salaam kinyume na matarajio ya wengi.

Baada ya timu hiyo kumeguka  kutokana na baadhi ya mastaa kuitwa katika timu zao za taifa mastaa waliobaki walipgwa na butwaa baada ya kupewa mapumziko ya siku moja pekee huku wakitakiwa kuripoti mazoezi Avic town mapema ambapo baada ya vipindi kadhaa vya mazoezi walihamia katika ufukwe wa Coco kujiweka fiti zaidi.

Kocha Yanga Miguel Gamondi akizungumza lengo kuu la kukipeleka kikosi chake ufukweni na kupiga tizi kwenye mchanga alisema ni kuongeza kasi na nguvu kwa wachezaji wake.

“Mara zote huwa naamini kuwa ushindi unaanzia mazoezini” Alisema kocha huyo raia wa Argentina ambaye amewakosha mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kushinda mechi za hivi karibuni kwa idadi kubwa ya mabao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala