Connect with us

Makala

Banda Apewa “Thank You” Simba sc

Winga Peter Banda ametemwa rasmi na klabu ya Simba sc ikiwa ni baada ya misimu miwili tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea  katika klabu ya Nyassa Big Bullet ya nchini kwao Malawi ambako pia alikua kwa mkopo akitokea klabu ya FC Sheriff Tiraspol ya nchini Moldovia.

Banda alitegemewa kuwa mmoja wa mastaa watakaofanya vizuri klabuni hapo lakini hata hivyo ameshindwa kufanya mambo makubwa tofauti na matarajio hasa akisumbuliwa zaidi na majeraha ya mara kwa mara kiasi cha kocha Robertinho kuamua kuachana nae.

Simba sc imeachana na Banda huku nafasi yake ikizibwa na Jose Luis Miqquisone ambapo pia msimu huu imefanikiwa kuwanasa baadhi ya mawinga kama Leandre Onana na Aubin Kramo ambao wanatarajiwa kufanya makubwa zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala